Sera na masharti ya chama

         

MASHARTI NA SERA YA MIKOPO YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO CHA SWISSPORT


 

SEHEMU YA KWANZA

 

1.0        JINA NA ANUANI

 

(a)  Jina la SACCOSS litakuwa Swissport Savings and Credit Cooperative Society Ltd

 

(b) Anuani:-    S.L.P. 18043 DAR ES SALAAM

 

 

(c)  Eneo la shughuli la SACCOS: TANZANIA BARA

 

 

(d)  Makao Makuu DAR ES SALAAM

 

 

(e)  Idadi ya wanachama waanzilishi kumi (10)

 

 

(f)   Fungamanisho la pamoja (Common Bond): wafanyakazi wa Fanyakazi wa mashirika ya Ndege Airport.

 

 

(g)  Tarehe ya kuandikishwa 25 novemba 2005

 

(h)  Nambari ya Kuandikishwa  KRL 649

 

 

 

 

 

 

 

SEHEMU YA PILI

 

2.0        TASWIRA, / MAHARUBU, MAADILI NA MISINGI YA SWISSPORT SACCOS.

 

2.1      TAASWIRA YA SWISSPORT SACCOS

 

            (SWISSPORT SACCOS VISION)

 

1.    Kuwa asasi kiongozi ya ushirika wa akiba na mikopo yenye kutoa bidhaa na huduma bora za fedha zinazohitajika na kutumiwa na wanachama / wateja.

 

2.2      MWELEKEO / MAHARUBU YA SWISSPORT SACCOS

            (SWISSPORT SACCOS MISSION)

 

Kuinua na kuendeleza SACCOS na wanachama wake wote kwa kutoa huduma na bidhaa mbalimbali muhimu za kifedha katika mazingira ya kiushindani yatakayoweza kumsaidia mwanachama kuondoa umaskini, kuheshimika na kutambulika katika hali iliyotawaliwa na haki chini ya misingi ya ushirika na ya kibiashara.

 

2.3      MAADILI YA SWISSPORT SACCOS

 

            (SWISSPORT SACCOS CORE VALUES)

 

Ushirika wa akiba na mikopo wa Swissport umejengeka katika maadili ya kujisaidia kuwajibika, demokrasia, usawa na haki. Wanachama huamini katika maadili ya ukweli, uwazi, uwajibikaji kijamii na kuwasaidia wengine.

 

 

2.4.     MISINGI YA USHIRIKA

 

(i)  UANACHAMA ULIO WAZI NA WA HIARI

 

Dhumuni muhimu la Swissport SACCOS ni kuhudumia wanachama na ikibidi wasio wanachama kwa hali ya juu na kwa busara. Katika kupokea wanachama Swissport SACCOS itapokea wanachama kwa kuzingatia uwazi na hiari bila kujali itikadi za kisiasa, udini, jinsia au ubaguzi wa kijamiaa bali mtu yeyote awezaye kuchangia na kuhitaji huduma zitolewazo na Swissport SACCOS.

 

            (ii)      UTAWALA WA KIDEMOKRASIA

 

Swissport SACCOS ni chama chenye kuongozwa kidemokrasia na kushirikisha wanachama wenyewe. Wanachama wote wanayo haki sawa katika upigaji kura kwa misingi ya mwanachama mmoja kura moja. Wanachama na watendaji budi washirikishwe kadri ya majukumu yao katika utoaji maamuzi na uwekaji sera.

 

            (ii)      USHIRIKISHWAJI WA WANACHAMA KATIKA SHUGHULI ZA KIUCHUMI

 

Wanachama wa Swissport SACCOS watachangia katika mtaji na kupata gawiwo kutokana na ziada itakayozalishwa.

Sehemu ya mtaji wa Swissport SACCOS utamilikiwa kwa pamoja kwa madhumuni ya kuendeleza malengo ya muda mrefu ya uhai wake.

Swissport SACCOS italipa faida juu ya mtaji kwa viwango vilivyoko kwenye soko, na baada ya kulipia gharama za uendeshaji.

Siada itayopatikana itagawiwa kama ifuatavyo:-

(a)  Maendeleo ya shughuli za Swissport SACCOS

(b) Faida kwa wanachama kufuatana na ushiriki wao katika shughuli za kiuchumi za Swissport SACCOS.

 

(iv)     ELIMU, MAFUNZO NA HABARI

 

Swissport SACCOS itachochea mipango ya utoaji elimu kwa wanachama, viongozi na watendaji ili kila mmoja aweze kujifunza kutoka kwa mwingine na kuweza kufundishana wenyewe kwa wenyewe katika kutimiza wajibu wo. Swissport SACCOS itaelimisha umma kuhusu uendeshaji na manufaa ya SACCOS.

 

 

 

 

            (V)      USHIRIKIANO NDANI YA USHIRIKA

 

Ili kuweza kutoa huduma bora kwa wanachama (SACCOS) na jamii kwa ujumla, Swissport SACCOS itakuza ushirikiano kati yake na vyama vingine vya ushirka ndani na nje ya nchi, kitaifa na kimataifa.

 

            (vi)     UHURU NA KUJITAWALA

 

Swissport SACCOS ni chama huru chenye kusaidiana na kudhibitiwa na wanachama wenyewe. Swissport SACCOS itafanya mikataba au kushirikiana na Serikali au Taasisi nyingine kwa hiari na uhuru na makubaliano yanayoihakikishia uhuru wa kujitawala katika maamuzi.

 

            (vii)    KUJALI JAMII

 

Swissport SACCOS itatoa huduma kw awanachama wake kwa kuzingatia jamii inayoizunguka. Katika kuhakikisha mahitaji ya wanachama ni budi kujali maendeleo ya jamii katika utengenezaji wa Sera na Masharti ambayo yataheshimu na kukubalika na wanachama, jumuia na mazingira.

 

SEHEMU YA TATU

 

3.        MADHUMUNI YA SWISSPORT SACCOS

 

Madhumuni ya Swissport SACCOS LTD ni kutoa huduma za kibenki kwa wanachama ili waweze kukidhi mahitaji mbalimbali ya kijamii na ya kiuchumi na kuinua hali ya maisha yao.

Swissport SACCOS LTD itafanya kazi zifuatazo ili iweze kutimiza na kufikia Taaswera, Maharubu, Misingi na madhumuni yake:-

a)    Kupokea kiingilio, Hisa, Akiba, michango ya Faraja na Amana, kutoka kwa wanachama na kutoa mikopo kwa wanachama.

b)   Kuweka viwango vya faida juu ya akiba na amana na riba juu ya Mikopo ya wanachama vinavyokidhi gharama za uendeshaji wa Swissport SACCOS LTD na kutoa manufaa kwa wanachama.

c)    Kupanga utaratibu unaofaa wa kutunza na kuweka kinga ya akiba na mikopo ya wanachama (Bima).

d)    Kuunda mtaji wa kutosha kuendesha shughuli za Swissport SACCOS LTD

e)    Kujenga tabia ya kuweka Akiba na Amana mara kwa mara na kukopa kwa busara na kulipa kwa wakati na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima miongoni mw wanachama.

f)     Kutoa elimu na mafunzo ya ushirika, ukimwi na mazingira kwa wanachama, viongozi na wafanyakazi wa Swissport SACCOS LTD (Watumishi).

g)    Kubuni utaratibu mzuri wa kutoa taarifa mbalimbali za shughuli za Swissport SACCOS LTD kwa wanachama na taasisi mbalimbali.

h)    Kununua Hisa na Dhamana kwenye vyombo vya fedha, serikali na Chama kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT), baada ya kujiunga na SCCULT.

i)     Kuhakikisha kuwa wanachama wanakuwa na makazi bora kwa kutumia mpango wa ujenzi wa nyumba bora (Housing Fund).

j)     Kufanya shughuli nyingine zozote halali za uzalishaji mali au biashara.

k)    Kuwezesha na kuongeza nguvu ya mtaji ili kupunguza UMASKINI miongoni mwa wanachama.

·         Kuwawezesha wanachama kupata mikopo yenye masharti nafuu kwa lengo la kuanzisha miradi mbalimbali, midogo na mikubwa ya kibiashara, kilimo na ufugaji.

·         Kuwawezesha wanachama kuanzisha ushirika ndani ya ushirika au vikundi vya kiuchumi miongoni mwao.

·         Kuwezesha wanachama na kuwajengea uwezo wa kutafuta masoko ya bidhaa zitokanazo na shughuli zao za uzalishaji mali.

·         Kusaidia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa jumla.

·         Kuwawezesha wanachama kuelewa na kufahamu kwa kina athari za UKIMWI na manufaa ya utunzani wa mazingira.

 

 

SEHEMU YA NNE

 

MAMLAKA YA SACCOS

 

4.        MAMLAKA YA SWISSPORT SACCOS LTD

 

            Swissport SACCOS LTD ina mamlaka yote ya:-

a)    Kufanya kazi na/au kuchukua hatua ya yoyote kwa makusudi ya kufikia Taaswira na Maharubu, na kutimiza madhumuni ya Swissport SACCOS LTD yaliyotajwa kwenye masharti haya.

 

b)   Kukopa, kukopesha na kudhibiti ulipaji mkopo kwa mwanachama asiyelipa mkopo kwa wakati uliopangwa na kumtoza adhabu kulingana na sera mikopo.

 

SEHEMU YA TANO

 

5.0      SIFA ZA MWANACHAMA

          a)       Awe mwenye umri wa miaka isiyopungua 18.

 

          b)       Awe mwenye tabia nzuri na akili timamu.

         

          c)       Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa au kuandikishwa na anayekubalika kwenye

masharti haya.

 

d)       Awe amelipa kiingilio, hisa na kuweka Akiba na awe anashiriki shughuli zote za Swissport SACCOS LTD.

 

e)       Awe tayari kufuata masharti ya Swissport SACCOS LTD na sheria ya vyama vya ushirika na marekebisho yake wakati wote.

 

f)       Kikundi au chama kinachoshughulika na shughuli zinazoambatana na shughuli za uchumi kinaweza kuwa mwanachama wa Swissport SACCOS LTD, ilimradi kiwe cha Tanzania Bara.

 

5.1      MAOMBI YA MWANACHAMA

 

Maombi ya mwanachama yatafanywa kwa maandishi kwa Halmashauri ya Swissport SACCOS LTD ambayo yatajadiliwa na ikiwa watayakubali itabidi mwanachama anayehusika athibitishwe na Mkutanao Mkuu.

 

Mwanachama akisha kubaliwa itabidi alipe kiingilio na kutoa angalau HISA mojai (1) na kukamilisha hisa 10 katika kipindi cha miezi 12. Na atakuwa akiongeza hisa, kuweka akiba mara kwa mara pamoja na Amana.

 

Swissport SACCOS LTD itakuwa na daftari ya uanachama yenye maelezo muhimu ya mwanachama kama vile jina la mwanachama, Namba ya uanachama, tarehe ya kupewa uanachama, hisa alizolipa, Hisa anazodaiwa, tarehe ya kuacha uanachama.

 

5.2      KUACHA NA KUSIMAMISHWA UANACHAMA

          a)       Mwnachama anaweza kuacha uanachama kwa taarifa ya maandishi.

 

          b)       mwanachama anaweza kusimamishwa uananchama kwa ajili ya:-

i)        Kushindwa kulipa mkopo wake katika muda ulioruhusiwa na Swissport SACCOS LTD pasipokuwa na sababu yoyote inayokubalika na kamati ya mikopo na kasha Halmashauri yote.

 

ii)       Kufanya kitendo chochote ambacho halmashauri itaridhika kuwa ni cha kutokuwa mwaminifu au kuwa na mwenendo ambao ni kinyume na maadili mema, mdhumuni, taaswira na maharubu ya Swissport SACCOS LTD. Kusimamishwa kwa sababu hii lazima kuthibitishwe na Mkutano Mkuu wa Mwaka.

 

iii)       Kusimamishwa kutahesabika tangu tarehe ya kutoa uamuzi wa kusimamisha mwanachama.

 

iv)      Kuacha kushiriki kshughuli za Swissport SACCOS LTD ikiwa ni pamoja na kutotekeleza maazimio ya mikutano mkuu.

 

c)    Uanachama utakoma kwa:-

i)             Kifo

ii)            Kuchukua hisa zake kwenye swissport SACCOS LTD

iii)           Ugojwa wa akili uliothibitishwa na Daktari aliyeandikishwa.

iv)           Kujiuzulu mwenyewe baada ya kutoa taarifa ya miezi mitatu (siku 90) kwa maandishi kwa swissport SACCOS LTD. Hata hivyo haki zake katika SACCOS hazitalipwa mpaka mahesabu ya SACCOS kwa kipindi hicho yawe yamekamilika na kukubaliwa na Mkutano Mkuu.

v)            Kuthibitisha kufukuzwa uanachama katika Mkutano Mkuu kwa kura ya Wanachama wasiopungua theluthi mbili (2/3) waliohudhuria, baada ya kupewa nafasi ya kujitetea kutokana na makosa ambayo yanasababisha kufukuzwa.

 
 

5.3      KUTEUA MRITHI

 

Kila mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa na haki ya kulipwa hisa na faida zote za Swissport SACCOS LTD. Mwanachma ana haki ya kubadilisha jina la mirth. Kila uteuzi utaandikwa katika daftari ya wanachama na mwanachama anayehusika atatia saini. Pia mirthi anaweza kurithi hisa na kuziendeleza shughuli kutegemeana na masharti ya Swissport SACCOS LTD wakati huo huo mrithi anawajibika kulipa madeni yoyote ya mwanachama kama yao.

 

5.4      HAKI NA WAJIBU WA MWANACHAMA

 

          Mwanachama yeyote atakuwa na haki na wajibu kama ifuatavyo:-

 

            5.4.1  HAKI KWA MWANACHAMA

 

i)        Kushiriki katika shughuli zote za Swissport SACCOS LTD kwa kufuata sheria ya ushirika iliyopo, kanuni ya ushirika, masharti ya Swissport SACCOS LTD, taratibu zote za uendeshaji (sera mbalimbali) na maazimio yote ya Mikutano Mikuu na Kawaida.

 

ii)       Kuhudhuria na kutoa maoni yake katika mikutano yote ya Swissport SACCOS LTD kwa mujibu wa sheria ya ushirika, kanuni za vyama vya ushirika na masharti haya.

 

iii)       Kuchagua na au kuchaguliwa kuwa kiongozi ili mradi ametimiza masharti na sifa zilizowekwa za uongozi mara kwa mara.

 

iv)      Kuweka na kutoa akiba, amana na hisa zake kwa kufuata kanuni za Swissport SACCOS LTD na kupata mikopo.

 

v)       Kuwa mdhamini wa mikopo kwa mwanachama mwingine yeyote wa Swissport SACCOS LTD.

 

vi)      Kupewa taarifa ya maendeleo ya Swissport SACCOS LTD. Kupewa masharti, kutazama mizania, mihutasarri ya mikutano mikuu na nyaraka za mrajisi wakati wa saa za kazi.

 

vii)      Kwa kushirikiana na wanachama wengine wasiopungua 1/3, atakuwa na haki ya kuomba kuitishwa kwa mkutano mkuu maalum kwa mujibu wa taratibu zinazosimamia uitishaji wa mkutano huo. (12.4.3).

 

viii)     Hakuna mwanachama yoyote wa Swissport SACCOS LTD atakayepewa au kutaka HAKI za Uanachama kabla ya kulipa kwenye Swissport SACCOS Hisa, Kiingilio na Michango mingine kama itakavyoamuliwa na mikutano mikuu.

 

 
            5.4.2  WAJIBU WA MWANACHAMA

 

i)        Kulipa kiingilio, kununua hisa na kuweka Akiba na Amana kwa mujibu wa masharti ya Swissport SACCOS LTD pamoja na kukopa kwa busara kulingana na mahitaji.
 

ii)       Kulipa mkopo katika muda uliopangwa kulingana na masharti ya Swissport SACCOS LTD.

 

iii)       Kulipa mkopo ulioudhamini endapo mkopaji atashindwa kulipa mkopo wake.

 

iv)      Kuwa mwaminifu kwa Swissport SACCOS LTD na kushiriki kikamilifu katika shughuli za swissport SACCOS LTD kuiwezesha Swissport SACCOS LTD kutimiza malengo yake.

 

v)       Kuhudhuria mikutano yote ya wanachama.

 

            5.4.3  WAJIBU WA SWISSPORT SACCOS

 

i)        Kutowabagua wanachama na kutenda haki kwa mujibu wa sheria na kanuni ya vyama vya ushirika na masharti haya.

 

ii)       Kuweka mazingira bora kwa mwanachama ya kuweka akiba, amana na kukopa kwa busara na kulipa kwa wakati uliopangwa.

 

iii)       Kutunga masharti na sera bayana kwa mwanachama kulingana na hali ya soko na utandawazi na mabadiliko ya mara kwa mara ya sayansi na teknolojia.

 

iv)      Kulinda maslahi ya wanachama.

 

v)            Kutafuta wanachama wapya kushirikiana na wana Swissport SACCOS LTD wengine.

 


SEHEMU YA SITA (6)

 

6.        KIINGILIO, HISA, AKIBA, AMANA NA FARAJA FUND.

 

6.1      KIINGILIO

 

Kila mwanachama lazima alipe kiingilio katika kipindi cha kukubaliwa kwake uanachama. Kiingilio hakirejeshwi kwa mwanachama akiacha uanachama au kusimamishwa uanachama na wala hakizai faida. Kiwango cha kiingilio kitapangwa kila mara na halmashauri kulingana na thamani ya shilingi ya wakati huo.

 

6.2      HISA

a)       Kila mwnachama atalazimika kuwa na hisa ndani ya SACCOS na idadi na thamani ya hisa vitapangwa na mikutano mikuu mara kwa mara.

 

b)       Mwnachama inabidi anunue hisa nyingi kwa faida yake mwenyewe nay a SACCOS yake lakini isizidi 1/5 ya hisa zote za Swissport SACCOS.

 

c)       Mwanachama anaweza kununua hisa moja au zaidi kwa wakati mmoja

 

d)       Kila mwanachama atapewa “Sahres certificate” na kuingizwa kwenye leja.

 

e)       Ili uwe mwanachama, mwanachama anatakiwa awe amenunua si chini ya hisa 1 na kuwa ametimiza kununua hisa zote 10 katika kipindi cha miezi 12.

 

f)       Mwnachama atakayeshindwa kununua hisa kufikia kiwango cha chini cha hisa, kinachotambulika kwenye SACCOS katika muda uliopangwa ataondolewa kwenye SACCOS. Kabla ya uongozi wa SACCOS kuchukua hatua hiyo, mwanachama atapewa taarifa ili ajirekebishe au kutoa sababu za msingi ambazo Halmashauri itaridhika nazo.

 

g)       Faida ya Swissport SACCOS inayopatikana kwenye shughuli zake zitagawiwa kwa mwanachama kulingana na hisa zao au itabaki kwenye Swissport SACCOS kuongeza hisa za wanachama na kutunisha mtaji wa Swissport SACCOS. Mgao huo utafanyika baada ya hesabu za Swissport SACCOS kukaguliwa na mizani kutolewa.

 

h)       Mwanachama akiachishwa uanachama anaweza kurudishiwa hisa na akiba pamoja na amana zake zote katika kipindi cha siku 30 iwapo hadaiwi na Swissport SACCOS.

 

i)             Deni la mwanachama kwa Swissport SACCOS halitazidi hisa zake ndani ya Swissport SACCOS. Iwapo mwanachama ana mkopo, hisa na amana, akiba zake zitachukuliwa kama dhamana ya mkopo.

 
 

6.2.1  KUUZA AU KUHAMISHA HISA

          a)       Hisa zinaweza kurithiwa, kuuzwa au kuhamishwa

 

b)       Hata hivyo Swissport SACCOS inaweza kununua hisa za mwanachama ambaye uanachama wake umekoma.

 

c)       Mwanachama akishindwa kukamilisha hisa zake zote katika kipindi kinachotakiwa hisa hizo zitahesabiwa kuwa zimefutika, hatarudishiwa

 

6.3      AKIBA

a)       Kila mwanachama lazima ajenge tabia ya kuweka akiba mara kwa mara kwa ajili ya mahitaji yake ya baadaye. (Kila siku, kila wiki, kila mwezi).

 

b)       Kila mwanachama ataweka walau kima cha chini cha akiba kila wiki, kila mwezi kama kiwango cha chini cha Akiba.

 

c)       Ili kuongeza Akiba ndani ya Swissport SACCOS kila mwnachama atapewa faida juu ya Akiba kila mwaka kadiri itakavyopangwa na Halmashauri kufuatana na hali halisi ya soko.

 

d)       Akiba za Mwanachama zitachukuliwa kama kigezo cha kupata mkopo mara mbili, tatu au zaidi kutokana na maamuzi ya Halmashauri kwa wanachama wanaokopa zaidi ya mara mbilikufuatana na uwezo wa kulipa.

 

e)       Akiba inatakiwa mfululizo zaidi ya miezi sita ili apate mkopo ila tu pale Swissport SACCOS inapokuwa na fedha za kutosha kwa mwanachama mpya.

 

f)       Kuweka akiba ni lazima katika Swissport SACCOS kila mwezi kwa kiwango kilichopangwa.

 

g)       Mwanachama anaweza kupunguza akiba yake kwa kiasi kisichozidi 20% ya akiba zake kwa kutoa taarifa kwa maandishi.

 

h)       Mwanachama anashauriwa kuweka akiba maalum za elimu (Education Savings Account), Afya (Health Savings Account), siku kuu, (Holidays Savings Account) na Mazishi (Funeral Account).

 

6.4.     AMANA

          a)       mwanachama anaweza kuweka Amana katika Swissport SACCOS na hii si lazima.

 

b)       Amana zinaweza kuchukuliwa muda wowote ule ambapo aliyeweka anahitaji kuchukua, na mwenye amana atapatiwa kitabu maalum cha amana.

 

c)       Kima cha chini cha kubaki kwenye Hesabu (Accont) kitakuwa kinapangwa na Halmashauri kwa niaba ya Mkutano Mkuu

 

d)    Amana zitakuwa zinapewa faida ya kiwango cha faida kitakachopagwa na Halmashauri kila mara kulingana na tahmani ya fedha.

 

6.5. FARAJA FUND

 

Kutaanzishwaanzishwa mfuko wa kufarijiana utakaoitwa Faraja Fund. Walengwa ni wafanyakazi wa Swissport DAR na watu wengine walio nje ya ajira ya Swissport. Lengo kuu la mfuko huu ni kutoa faraja ya kifedha kwa Mfiwa/wafiwa.  Mfiwa atapata huduma kutoka katika mfuko huu iwapo tu ana mahusiano ya damu na marehemu  au ni mke au mume wa marehemu.  Mahusiano ya damu kwa maana ya kwamba ni mtoto, baba au mama. Kwa siku za usoni tunaweza kupanua wigo wa mfuko na kuingiza masuala mengine kama ya sherehe ndani ya mfuko. 

Masharti ya Uendeshaji Mfuko.

  1. Mwanachama atajaza fomu maalumu ya kuomba kujiunga na mfuko kutoka  ofisi za Swissport Saccos.
  2. Kiwango cha mchango kwa kila mwanachama kitakuwa Tsh.10,000 kwa mwezi na itakatwa kwenye mshahara.
  3. Michango itakayofanywa hapo juu haitarudishwa iwapo mwanachama atajitoa kwenye mfuko bila kujalisha kama alishawahi nufaika na mfuko au la.
  4. Mwanachama atalipwa fedha kwa Mkupuo Tsh. 500,000/= akifiwa na mume, mke, au mtoto na Tsh 1,000,000/= italipwa kwa mrithi (beneficiary) wa mwanachama iwapo mwanachama mwenyewe atafariki.
  5. Mfuko utaanza kutoa huduma baada ya miezi mitatu tangu kuanzishwa. Tunatarajia kuuzindua mfuko mwezi wa kumi hivyo wanachama wataanza kunufaika kuanzia mwezi wa Januari 2012
  6. Wanachama wote watakaojiunga na mfuko baada ya October 2011 itawalazimu kukaa miezi sita ndipo waanze kupewa mafao ya mfuko huu.
  7. Mfuko unatoa fursa ya uanachama hata kwa wasio wanachama wa Swissport Saccos
  8. Mwanachama atakayebainika kutoa taarifa za uongo au udanganyifu wowote ili apate sifa ya kuhudumiwa na mfuko huu, atatakiwa kurejesha fedha yote aliyopewa kama faraja pamoja na riba kwa mujibu wa viwango vya ukokotoaji wa riba kutoka Swissport Saccos.

9.    Ni wajibu wa mwanachama kutoa vielelezo vinavyojitosheleza kwa uongozi ili aweze kuhudumiwa kwa muda muafaka.

 

10. Meneja wa chama ataandaa na kuweka kumbukumbu za mfuko huu kwa uhakiki/ tathmini na utekelezaji wake utapitiwa na bodi mara kwa mara.

 

11. Kiwango cha uchangiaji kwenye mfuko wa faraja kitabadilishwa na wanachama pindi itakapoonekana haja ya kufanya hivyo.

 

12. Kumbukumbu za Mwajiri zitatumika kubaini mahusiano yaliyotajwa katika aya ya utangulizi

 

SEHEMU YA SABA (7)

 

7.        MIKOPO KUTOKA TAASISI ZA FEDHA

a)       Swissport SACCOS inaweza kukopa kutoka taasisi zingine baada ya kupata idini ya halmashauri kwa maslahi ya wanachama wote kulingana na masharit ya wakopeshaji.

i)        Kiasi kisichozidi robo (1/4) ya jumla ya hisa zote pamoja na akiba, amana, kwa uamuzi wa angalau robo tatu (3/4) ya wajumbe wa Halmashauri.

 

ii)       Kiasi zaidi kinaweza kukopwa baada yakupata  uamuzi wa wanachama kwenye mkutano mkuu ambao wataafiki pendekezo lililofanywa na robo tatu (3/4) ya wajumbe wa Halmashauri.

 

b)       Dhima ya mwanachama kwa ajili ya madeni ya SACCOS haitazidi kiwango cha hisia zake ndani ya SACCOS.

 

SEHEMU YA NANE (8)

 

8.        VYANZO VYA FEDHA, MATUMIZI NA UWEKEZAJI

            8.1      VYANZO VYA FEDHA VYA SWISSPORT SACCOS

 

                   a)       Akiba na amana za wanachama

                   b)       Amana kutoka wanachama

                   c)       Michango maallum, ruzuku na misaada.

                   d)       Ziada halisi

                   e)       Mikopo kutoka mabenki na taasisi nyingine za fedha      

                   f)       Michango ya mara kwa mara kama itakavyoamuliwa na mkutano mkuu.

                    g)       Shughuli halali za kibiashara.

 

            8.2      MTAJI WA SWISSPORT SACCOS

                   a)       Hisa za wanachama

                   b)       Ziada halisi

                   c)       Akiba ya lazima na malimbikizo

                   d)       Michango maalum, ruzuku na misaada.

                            

                             MATUMIZI YA FEDHA

                             Fedha za Swissport SACCOS zitatumika kwa shughuli za maendeleo ya

SACCOS ili kiweze kutimiza madhumuni yake kulingana na masharti haya.

            8.3      UWEKEZAJI

                        DAHACO SACCOS ITAHIFADHI FEDHA ZAKE KWA:-

a)    Kuweka akiba na amana benki na kununua amana za serikali.

i)             Mahitaji ya mikopo ya wanachama yakitoshelezwa, fedha ambayo itazidi inaweza kuwekwa sehemu nyingine yeyote itakayowapatia faida kubwa zaidi.

ii)            Fedha yote ya SACCOS isipokuwa ile inayohitajika kwa matumizi madogo madogo itahifadhiwa benki. Kamati itaamua kiasi cha fedha kitachobaki kwa matumizi madogo madogo na kwa ajili ya Hesabu ya amana.

b)   Kutoa mikopo kwa wanachama na vikundi vya wanachama.

c)    Kununua hisa kwenye vyombo vya fedha na makampuni n.k. iwapo kutakuwa na fedha za ziada.

d)    Fedha za SACCOS lazima ziwekewe kinga dhidi ya majanga.

 

SEHEMU YA TISA (9)

 

9.        HESABU ZA SWISSPORT SACCOS

a)       Mwaka wa fedha wa chama utakuwa kuanzia tarehe 1 January hadi tarehe 31 December kila mwaka.

 

b)       Swissport SACCOS itandika vitabu vya hesabu na kutunza kumbukumbu muhimu kulingana na maelekezo ya mrajis wa vyama vya ushirka na kanuni za uhasibu za kimataifa.

 

c)       Hesabu za Swissport SACCOS zitafungwa kila siku na urari wa mahesabu utatolewa.

 

d)       Halmashauri ya Swissport SACCOS itapita mfumo wa hesabu na utunzaji kumbukumbu za Swissport SACCOS kila mwaka kwa kushirikiana na mkaguzi wa Swissport SACCOS. Wajumbe wa kamati ya usimamizi wanaweza kuchunguza vitabu na kumbukumbu za Swissport SACCOS wakati wowote kwa kushirikiana na maafisa ushirika na maofisa wa SCCULT pamoja na wataalamu wentine kulingana na maamuzi ya halmashauri.

 

e)       Vitabu vya Swissport SACCOS ya vyama vya ushirika, na mkaguzi yeyote atakayekubalika.

 

f)       Gharama za ukaguzi zitalipwa na Swissport SACCOS yenyewe.

 

g)       Swissport SACCOS itakuwa na Accounting manual na utaratibu maalum wa fedha (“Swissport SACCOS Financial Regulations”).

 

9.0      MGAO WA ZIADA (MGAO WA WANAHISA/ WANACHAMA)

Halmashauri ya Swissport SACCOS itatoa mapendekezo ya mgao wa ziada ya mwaka uliopita kwenye Mkutano Mkuu wa Swissport SACCOS kwa wanachama wote. (wanahisa).

a)    Kila mwaka Swissport SACCOS itatenga kiasi kisichopungua asilimia (20%) kutokana na faida halisi kwa ajili ya akiba ya lazima. Akiba ya lazima itabakia kuwa ni mali ya SACCOS na haitwezekana kugawanywa isipokuwa kama Swissport SACCOS itavunjwa. Viingilio vyote, adhabu mbalimbali na gahrama za uhamisho wa Hisa zitaongezwa katika akiba hii baada ya kutoa garama za kuandikishwa Swissport SACCOS.

b)   Asilimia kumi (10%) ya faida kwa ajili ya mfuko wa elimu.

c)    Asiimia kumi (10%) kwa ajili ya mfuko wa kukombolea hisa za walioacha uanachama lakini kiasi hicho kisizidi asilimia kumi (10%) ya hisa zote.

d)    Asilimia kumi (10%) ya faida halisi itatengwa kwa ajili ya kinga ya madeni mabaya. Lakini kiasi hicho kisizidi asilimia kumi (10%) ya madeni yote.

e)    Asilimia kumi (10%) au zaidi kwa ajili ya maendeleo ya SACCOS.

f)     Mgao wa ziada wa wanachama kulingana na hisa alizonazo mwanachama. Ikiwa Swissport SACCOS inahitaji kukuza mtaji na kuwekeza rasilimali, kiasi hicho cha mgao kitaongezwa kwenye hia za wanachama.

g)    Kwa idhini ya mkutano Mkuu Halmashauri ya Swissport SACCOS inaweza kupewa tuzo.

h)    Ziada itagawanywa tu baada ya vitabu vya mahesabu kufungwa na mizani iliyokaguliwa kutolewa, na hesabu ya mgao kuidhinishwa na Mrajisi wa vyama vya ushirika.

 

SEHEMU YA KUMI (10)

 

10.0   TARATIBU ZA UWEKAJI AKIBA NA AMANA

10.1   TARATIBU ZA KUWEKA AKIBA

a)       Kila mwanachama atapatiwa kitabu cha akiba (Pass Book) ambacho kitaonyesha kiasi cha akiba na mikopo, kiasi alichokopa na baki ya akiba na mikopo.

b)       Vitabu vya Akiba vitakuwa na namba zinazofuatana na mara moja kutolewa kwa wanachama. Namba za vitabu hivi zitaandikwa katika daftari za wanachama na kadi/leja ya mwanachama.

c)       Fehda yote ya mwanachama inayopokelewa ndani ya Swissport SACCOS itakatiwa stakabadhi ya fedha na kuingizwa katika kitabu chake (Pass Book) na kutiwa saini na mweka hazina au mtu mwingine aliyeidhinishwa kupokea fedha, kasha kitabu hicho atapewa mwanachama mwenyewe akitunze.

d)       Ikiw kitabu kitapotea mwnachama anayehusika atawajibika kutoa taarifa ya maandashi kwa mweka hazina na Meneja. Kamati ya Utendaji inaweza kuidhinisha kitabu kingine kitolewe na mwenye kitabu atalipa ada ya kitabu kipya kadri itakavyoamuliwa na kamati ya utendaji. Kitabu kipya kitaingizwa salio za hesabu zote za mwanachama kama zilivyo kwa tarehe anayopatiwa kitabu kipya.

e)       Kitabu cha akiba hakina budi kionyeshwe wakati wote wa kuweka fedha au wakati wa kuchukua mkopo au akiba ili mhasibu aweze kuingiza kiasi kilichowekwa au kuchukuliwa.

f)       Akiba zinaweza kuwekwa kwa fedha taslimu au hundi na mwanachama anawezakumuagiza mtu mwingine kumuwekea akiba zake lakini siyo kumchukulia ila kwa maandishi maalum.

g)       Kutakuw na kiwango cha chini cha akiba kwa kila mwanachama.

h)       Kutakuwa na akiba za kawaida ambazo zinafahamika kama njia ya kukopea na dhamana za mikopo ikopywayo, na akiba maalum za hesabu ya elimu, afya, sikukuu. N.k.

i)        Akiba zitapewa faida kama itakavyopangwa mara kwa mara na halmashauri kulingana na hali ya soko.

 

10.2   UTARATIBU WA KUWEKA AMANA

a)       Kila mwanachama anaruhusiwa kuweka amana na kuchukua muda wowote anaohitaji ndani ya muda wa saa za kazi.

b)       Kutakuwa nauwekaji wa amana maalum. (ya miezi mitatu, sita, mwaka hadi miaka miwili) (FIXED DEPOSIT).

 

SEHEMU YA KUMI NA MOJA (1)

11.0   SERA NA TARATIBU ZA MIKOPO

            A:        SERA YA MIKOPO

i)        Sera ya Mikopo ya Swissport SACCOS LTD itakuwa ni kutoa huduma kwa wanachama wake ya kuweka AKIBA za kifedha, nafasi za uwekezaji na mikopo wkati inapohitajika.

ii)       Swissport SACCOS LTD itatoa mikopo kwa:-

1)    Wanachama mmoja, kikundi kimoja mwanachama wa SACCOS kulingana na mahitaji yao na uwezo wao wa kulipa.

2)    Wanachama au kikundi kimoja ambacho kina utawala wa kadiri kwenye miradi yao au yake ili kupunguza majanga na uchelewashaji wa mikopo.

3)    Kwa wanachama ambao wanataka kuanzisha miradi midogo midogo au mikubwa watapewa nafasi ya kwanza.

4)    Kwa ajili ya kuendeleza ubora wa Afya, maisha na Elimu ya mwanachama na familia yake itapewa nafasi ya PILI

 

iii)       Utaratibu wa utoaji mikopo kwa Swissport SACCOS LTD utakuwakutoa mkopo siyo zaidi ya miezi 24 kwa ajili ya kuweka masuala ya mzunguko wa fedha vizuri. Mwanachama atakuwa na haki ya kukopa mara mbili ya baki ya AKIBA yake au kulingana na uwezo wake wa kulipa. Lakini mara zote kigezo ni mara mbili ya AKIBA za mwanachama. Na mikopo itakuwa inapitishwa na kamati ya mikopo mara moja kwa mwezi kwa mikopo ya miradi na maendeleo. Utaratibu utakaotumika ni aliyekuja kwanza kupewa kwanza (FIRST COME FIRST SERVED BASIS).

 

          Viwango vya faida juu ya mkopo vitakuw vinatozwa na kupata kila mwezi kw amtindo wa kupunguza kwa baki ya mkopo. Viwango vinaweza kubadilishwa kwa taarifa fupi kwa sababu ya kukua kwa kshughuli au kwa sababu ya kubadilika kwa viwango vya biashara. Mara maombi ya mkopo w mwanachama yatakapo idhinishwa fomu ya makubaliano itasainiwa na kuonyesha mpango wa ulipaji itakayoonyesha riba itakayotozwa (interest charged), muda wa mkopo na marejesho ya kila mwezi, au marejesho toka tarehe atakayo elekezwa kuanzakulipa. Baada ya hapo fedha taslimu au hundi itatolewa kwa mwanachama. Haitegemewi kwamba wanachama watakopa mikopo kwa ajili ya vifo, harusi, sherehe za kipaimara, unyago au ngoma.

 
 

B.        SERA YA UTOAJI MIKOPO

i)        Mikopo itatolewa kwa mtu au kikundi ambacho ni mwanachama wa Swissport SACCOS LTD.

 

ii)       Mikopo itatolewa kwa mwanachama hai wa Swissport SACCOS LTD aliyetoa kiingilio, HISA na kuweka Akiba na kulipa michango ya kila mara.

 

iii)       Mikopo itatolewa kwa kikundi ambacho kinaeleweka na Swissport SACCOS LTD vizuri hususani vikundi vya wanachama.vikundi hivyo ni lazima view na watu wasiopungua watano watano, na vikundi vya wanawake vitapewa kipaumbele.

                  

                        C.        UTARATIBU WA UTOAJI MIKOPO

i)        Maombi yote ya mikopo katika Swissport SACCOS LTD ni lazima yafanyike katika fomu maalum na ni lazima kwa kila hali fomu ielezee kiasi cha mkopo kilichoobwa, madhumuni ya mkopo muda wa mkopo na dhamana ya mkopo.

 

ii)       Maombi ya mkopo kwa hatua za mwanzo ni lazima ipitiwe na Afisa Mikopo au na Mhasibu na maombi yao yatapelekwa kwenye kamati ya Mikopo kw ahatua ya mwisho ya kuidhinisha.

 

iii)       Kutegemeana na upatikanaji wa fedha, maombi ya mikopo yatafuata utaratibu wa aliyekuja kwanza kuhudumiwa kwanza. Wakati maombi ya mikopo yanazidi fedha zilizopo, kipaumbele kitatolewa kwa ajili ya mikopo yenye kiasi kidogo. Hata hivyo, wakati maombi ya mikopo yanakaribia kuwa sawa na mikopo itakayojadiliwa katika hatua zifuatazo:-

·         Mwnachama au kikundi ambacho hakijapata mkopo kabla.

·         Mwanachama au kikundi kipya ambacho ndiyo kwanza kinatakiw akupata mkopo.

·         Mwnachama au kikundi ambacho kimemaliza kulipa vizuri mkopo uliotangulia na akaomba mkopo mpya.

 

iv)      Kiasi cha juu cha mkopo kitakachoteolewa kwa mwanachama kitajadiliwa na kamati ya mikopo kila mara, mara mbili ya AKIBA za mwanachama au kikundi kulingana na uwezo wa kulipa. Labda mkopo ulioombwa ni sawa au kidogo kulinganishwa na AKIBA zilizowekwa, mkopo unaweza kuidhinishwa na Afisa Mikopo na Muhasibu.

v)       Ni kwa wale wanachama au vikundi pekee vilivyotimiza wajibu wao ipasavyo kwa Swissport SACCOS na walioweza kutosheleza matakwa ya Kamati ya Mikopo watakuwa na haki ya kupokea mikopo kutoka kwenye Swissport SACCOS LTD.

vi)      Mikopo inaweza kutolewa kwa fedha taslimu, hundi au vifaa kama itakavyoombwa na mwanachama mkopaji au ifakavyoamuliwa na Kamati ya Mikopo.

           

D:        MIKOPO ITATOLEWA KWA AJILI YA MADHUMUNI YAFUATAYO:

Kipaumbele cha juu kitatolewa kwa mikopo inayoelekezwa kwenye shughuli za maendeleo katika sehemu tatu.

·         Mikopo ya maendeleo ya kiuchumi, Uvuvi, Biashara kubwa na ndogo ndog, kilimo na ufugaji, Kipaumbele kitatolewa kwa wale wenye shughuli tayari.

·         Mikopo ya maendeleo ya kukuza hali ya maisha, kamavile Elimu, Afya Ujenzi wa Nyumba, Ununuzi wa Vifaa (ndani ya nyumba, usafi nk).

·         Mikopo kwa ajili ya majanga / dharura.

 

E:         ULIPAJI

          Muda wa ulipaji utategemeana na aina ya mkopo uliotolewa.

          i)        Mikopo ya maendeleo ya kiuchumi kwa wanachama italipwa    kwa muda usiozidi miezi ishirini na nne (24).

 

ii)       Mikopo ya Maendeleo ya kukuza hali ya maisha ya wanachama italipwa kwa muda usiozidi miezi kumi na mbili hadi miezi kumi na nane (12-18).

 

iii)       Mikopo ya majanga kwa muda usiozidi miezi sita (6) Mwanachama anaweza kuwa na mikopo ya aina mbili yaani mkopo wa maendeleo ya kiuchumi na kukuza hali ya maisha au na majanga / dharura maisha na majanga.

 

            F:         DHAMANA YA MKOPO

i)        Labda mkopo ulioombwa ni sawa au chini ya AKIBA zilizowekwa na mwanachama, mkopo ni lazima uwekewe dhamana.

 

ii)       HISA na AKIBA zilizowekwa ndani ya Swissport SACCOS LTD na mwanachama zitachukuliwa kama dhamana ya mkopo wa mwnachama; au kamati ya Mikopo itatoa mapendekezo kwa mwanachama kuwwekeza HISA na AKIBA zingine kama itaona inahitaji dhamana ya kudhamini mkopo kwa njia ya HATI kama vile share certificate na Title need hasa kwa mikopo itakayokopeshwa kulingana na uwezo wa kulipa.

·         HISA na AKIBA hizo hazipaswi kuondolewa labda kama baki ya mkopo ni sawa au ipo chini ya jumla ya AKIBA.

 

iii)       Mali yoyote iliyonunuliwa na mwanachama kupitia fedha za mkopo wa Swissport SACCOS LTD itachukuliwa kama dhamana ya mkopo (mfano: samani, jingo, vifaa nk.).

 

iv)      MALI nyingine za mwanachama zitachukuliwa na Kamati ya Mikopo kama dhamana kwa ajili ya mkopo. Hii itahusisha AKIBA, AMANA, MAJENGO nk.

 

v)       Iwapo kumetokea ucheleweshaji wa urejeshaji mkopo Swissport SACCOS LTD italazimika kuchukua MALI za mwanachama baada ya WADHAMINI wake hao kushindwa kulipa mkopo na kuchukua hatua kwa mujibu wa taratibu zilizopo yaani sheria ya ushirika, masharti ya Swissport SACCOS LTD na sheria zilizopo za nchi.

vi)      Kwa mikopo ya vikundi kikundi chochote kitakuwa ndiyo dhamana na utaratibu wa “group lending” na “affidavit” utatumika.

 

            G:        KUJADILIWA KWA MAOMBI YA MIKOPO

i)        Maombi ya mikopo yatajadiliwa katika vikao halali vitakavyofanywa na Kamati ya Mikopo ya Swissport SACCOS LTD kwa akiba iliyotakiwa. Hakuna mwanakamati atakayedili maombi yake ya mkopo.

 

ii)       Kamati ya Mikopo inaweza kuchukua HATUA zifuatazo katika MAOMBI YA MKOPO:-

·         Inaweza kuidhinisha mkopo kw amasharti tofauti kulingana na ilivyokuwa kwenye maombi ya mkopo. Marekebisho yatakayofanywa na Kamati ya Mikopo yanaweza kuhusisha kiasi cha mkopo, muda wa marejesho, mahitajio ya dhamana n.k. nah ii ni lazima ifanywe na kamati iliyotimia akidi. (quorum).

·         Kamati ya mikopo inaweza kutofautiana katika kujadili maombi ya mkopo hadi hapo masharti Fulani yatakapotimia au kuomba taarifa za nyongezakutoka kwa mwanachama au watendaji n.k.

 

iii)       Kama mkopo haukuidhinishwa au kujadiliwa kwasababu za hapo juu,

maombi yatakuwa yamekataliwa.

                  

                   iv)      Kamati ya mkopo inatakiwa kuweka kumbukumbo zote za vikao ambazo

zitakuwa na:-

·         Tarehe, muda na mahali palipofanyika kikao na majina ya wajumbe wote walioshiriki kikao.

·         Orodha ya maombi yote ya mkopo yaliyotakiwa kujadiliwa kwenye kikao.

·         Mikopo iliyoidhinishwa ikiwemo kiasi, muda, jinsi ya kulipa na maelekezo maalumu kuhusiana na mkopo. Kama kamati itabadilisha chochote kabla ya kuidhinisha ni lazima nayo iwemo.

·         Mikopo iliyokataliwa maelekezo yake maalum na mapendekezo yake yatapelekwa kwa mwanachama husika.

·         Matokea ya mapitio yote ya maombi ya mikopo n.k. lazima yawekwe kwenye kumbukumbu.

·         Wajumbe wote wa kamati waliokuwepo na waliojadiliw ni lazima waweke saini zao.

 

vi)           Fomu zote za maombi ya mikopo zitaidhinishwa na kiongozi wa karibu aliyeteuliwa kuidhinisha maombi ya wanachama walioko kwenye eneo lake kwa kuzingatia utaratibu wanachama walioko kwenye eneo lake kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa ndani ya masharti haya au mtendaji wa kata anakoishi mkopaji.

vii)          Mikopo yote ni lazima iwekewe bima ya mikopo kupitia kwenye utaratibu wowote wa bima kama ilivyo kwenye kanuni ya vyama vya ushirika namba 85.

 

H:       Urejeshaji wa mikopo utafanywa kwa kulipa fedha taslimu au hundi kwatika ofisi       

Ya Swissport SACCOS LTD wakati w asaa za kazi, au muda mwingine utakaopagwa.

 

I        Mkopo utatozwa riba kiwang cha riba juu ya mkopo kitaamuliwa Halmshauri na kulingana na gharama za uendeshaji. Riba ya mkopo itatofautiana kulingana na aina ya mkopo na muda wa urejeshaji.

 

J.       Baadha ya mkopo kuidhinishwa mkopaji atajaza fomu maalum ya mkataba (loan agreement form) ambayo itatiwa saini na wadhamini hao wawili. Fomu hii itaonyesha masharti ya mkopo.

 

K.       Maombi ya Mwanakamati wa mikopo yatajadiliwa na wanakamati waliobaki ili mradi akidhi itimie.

 

L.       Kama Swissport SACCOS LTD imepata mkopo toka sehemu nyengine itakopesha kulingana na masharti ya mkopo huu. (Mfano – faida au jinsia).

 

SEHEMU YA KUMI NA MBILI (12)

UONGOZI NA USIMAMIZI

 

12.0   UONGOZI

12.1    a)       Swissport SACCOS LTD  itaongozwa na Halmashauri ambayo itaundwa na

wajumbe wasiopungua wanne na wasiozidi kumi na tano ni pamoja na mwenyekiti na makamu wake.

 

b)       Wajumbe wa Halmashauri watachaguliwa na mkutano mkutano mkuu wa Swissport SACCOS LTD na muda wao wa ofisi utakuwa miaka mitatu lakin wanaweza kuchaguliwa tena na kila mwaka 1/3 ya Halmashauri itajiuzulu.

 

c)       Halmashauri ya Swissport SACCOS LTD itagawawanyika katika kamati tatu ambazo wajumbe wake nao ni lazima wachaguliwe kwenye mkutano mkuu nazo ni:-

·         Kamati ya Utendaji

·         Kamati ya Mikopo

·         Kamati ya Usimamizi

Halmashauri inaweza kuunda kamati zingine ndogo na kuteua wajumbe kulingana na mahitaji miongoni mwa wanachama, halmashauri na wataalamu wengine nje ya SACCOS.

 

            12.1.2            UCHAGUZI WA HALMASHAURI

Uchaguzi wa Halmashauri utafanyika kwa mujibu wa sheria na Kanuni ya vya vyama vya ushirika.

 

Hatua zifuatzo zitafuatwa wakati wa uchaguzi wa Halmashauri:-

a)    Inapofika agenda ya uchaguzi wa viongozi, Mrajis Msaidizi / Afisa Ushirika au mtu mwingine anayekubalika kisheria wa eneo la Swissport SACCOS LTD atasimamia. Mkutano utachagua Mwenyekiti atakayeongoza uchaguzi, mwenyekiti khyo sharti atokane na miongoni mwa wajumbe wa Mkutano Mkuu.

b)   Idadi ya wanachama watakaogombea nafasi ya ujumbe wa Kamati itapendekezwa na Mkutano Mkuu kutokana na mapendekezo kuungwa mkono na angalau mwanachama mmoja kwa kila mgombea kutoka miongoni mwa mwanachama waliohudhuria mkutano huo.

c)    Uchaguzi wa idadi yote ya Halmashauri utafanyika kama ifuatavyo:-

i)   Mapendekezo ya jina la mgombea nafasi ya ujumbe wa kamati utafanyika kwa kuonyesha mkono na kuugwa mkono na angalau mwanachama mmoja kutoka miongoni mwa wanachama waliohudhuria mkutano huo.

 

ii)  Uchaguzi wa Mjumbe wa Kamati utafanywa kwa kupigiwa kura ya siri tu na wala siyo vinginevyo.

 

iii)           Mara tu baada ya uchaguzi, kura zitahesabiwa na matokeo kutangazwa na Mwenyekiti wa Mkutano.

 

d)    Uchaguzi wa mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu na Mtunza Hazina utafanywa moja kwa moja na Mkutano Mkuu.

 

e)    Uchaguzi wa Kamati ya utendaji, Mikopo na Usimamizi utachaguliwa na Mkutano Mkuu. Kila nafasi itachaguliwa pekee kwenye mkutano Mkuu na kasha kuunda Halmashauri.

 

f)     Nafasi ya Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti au Halmashauri yeyote iwapo itagombewa na mtu mmoja bila upinzani kura za siri lazima zipigwe za ndivyo au hapana.

 

Kiongozi wa halmashauri ya Swissport SACCOS ni lazima awe na sifa zifuatazo:-

i)   Awe amekaa ndani ya SACCOS siyo chini ya mwaka mmoja isipokuwa

wakati wa kuanza chama.

ii)  Asifanye shughuli zinazofanana na zile zinazofanywa na Swissport  SACCOS.

iii)  Asiwe kiongozi wa chama chochote cha SIASA.

iv) Awe na kiwango cha elimu ya angalau Sekondari.

V) Awe amekamilisha hisa zake zote na kuweka akiba za kila mara na michango mingine yote kama ilivyoamuliwa na mikutano mikuu ya wanachama.

 

12.2   AINA YA MKUTANO

            12.2.1            MKUTANO MKUU WA MWAKA

a)       Mkutano mkuu wa Mwka wa Swissport SACCOS LTD utafanyika mara baada ya kufunga mwaka wa Swissport SACCOS LTD na isizidi miezi mitatu baada ya mwisho wa mwaka wa hesabu, mahudhurio ni suala muhimu, katika kila mkutano inabidi kuthibitisha kama idadi ipasayo ya mahudhurio imetimia.

b)       Mahudhurio ya Mkutano Mkuu yasipungue nusu (1/2) ya wanachama wote au wanachama mia (100) idadi yoyote iliyo ndogo itachukuliwa. Idadi isipotimia Mwenyekiti ataahirisha mkutano na kupanga siku nyingine ya kufanya na idadi yoyote itafanya mkutano kuwa halali. Uwakilishi utahesabika kwa wanachama walio mbali na makao makuu.

 

c)       Mambo yafuatayo lazima yajadiliwe katika Mkutano Mkuu wa mwaka:-

i)        Kusoma na kuthibitisha mambo ya Mkutano Mkuu uliopita na yatokanayo.

ii)       Taarifa za:-

a)    Mwenyekiti

b)   Mweka Hazina / Meneja wa saccos

 

iii)       Kujadili taarifa ya ukaguzi wa Mrajis na kukubali au kukataa taarifa ya mwaka ya mahesabu ya mizania.

 

iv)      Kufanya uchaguzi wa wajumbe wa kamati mbalimbali za Swissport SACCOS LTD ikibidi kusimamisha na kufukuza baadhi yao.

 

v)       Kujadili namna ya kugawana ziada kwa kuzingatia masharti ya Swissport SACCOS LTD, kanuni na sheria ya vyama vya ushirika.

 

vi)      Kujadili mapendekezo ya miradi ya Swissport SACCOS LTD na kutoa maamuzi.

 

vii)      Kuidhinisha ununuzi au uuzaji wa mali ya Swissport SACCOS LTD yenye thamani kama inavyoruhusiwa na sheria ushirika.

 

viii)     Kuzungumzia mambo mengine yanayohusu maendeleo ya Swissport SACCOS LTD kwa jumla na kutoa maelekezo ya utekelezaji kwa Halmashauri.

 

ix)      Kufikiria kiwango cha honoraria kwa ajili ya Halmashauri.

 

x)       KUweka kiwango cha riba jumla ya mikopo na faida juu ya amana na akiba.

xi)      Kuweka idadi ya hisa na thamani ya hisa moja.

xii)      kubadilisha au kufany marekebisho yoyote katika masharti haya kama ilivyo kwenye sheria ya vyama vya ushirika.

xiii)     Kujadili mapendekezo ya sera mbalimbali za Swissport SACCOS LTD.

xiv)     Kujadili wanachama wapya na wanojitoa.

 

            12.2.2            MIKUTANO MIKUU YA KAWAIDA

a)       Kutakuwepo na Mikutano Mikuu ya kawaida miwili ambayo itafanyika wakati wowote katika mwaka wa fedha wa SACCOS iwapo itakuwa lazima kufanya hivyo.

 

b)       Mambo yafuatayo yatajadiliw katika Mkutano Mkuu wa Kawaida:-

          i)        Kuthibitisha muhtasari wa mkutano uliopita nayatokanayo.

          ii)       Kujadili na kufikiria taarifa za maendeleo ya utekelezaji kutoka

kwa kamati ya utendaji, mikopo nay a usimamizi.

iii)       Kuthibitisha kuingizwa au kufukuzwa kwa mwanachama.

iv)      Kuidhinisha makisio ya mapato na matumizi ya mwaka unaofuata.

v)       Kuweka ukomo wa madeni chini ya sheria ya vyama vya ushirika.

vi)      Kuzungumzia mambo yote yanayohusu maendeleo ya Swissport SACCOS LTD kwa jumla na kutoa maelekezo ya utekelezaji kwa halmashauri. Hata hivyo wanachama waliohudhuria mkutano wowote wanaweza kuamua kubadilsisha kwa muda mambo yatakayozungumzwa kwa kura ya 2/3 ya wajumbe.

 

C)       Katika kupang amikutano mikuu ya kawaida, itabidi mkutano ufanyike angalau miezi miwili kabla ya kufunga hesabu za chama kwa ajili ya kujadili 12:4:1 c(v) na (Vii).

 

            12.2.3            MKUTANO MKUU MAALUM

a)       Mkutano Mkuu Maalum utafanyika wakati wowote iwapo utaiitishwa na Mrajis wa vyama vya ushirika au mtu aliyeruhusiwa na Mrajis au kwa maombi ya maandishi ya wanachama wasiopungua theluthi moja (1/3.

 

b)       Mkutano Mkuu Maalum ukiombwa na wanachama, maombi ni lazima yataje sababu za kutaka mkutano huo ufanyike na waombaji lazima waweke saini zao na wapeleke maombi hayo kwa mwenyekiti wa chama na nakala kwa Afisa ushirika, na ni lazima wawe wanachama hai tu. (Active members).

 

12.3   KUITISHA MKUTANO MKUU

a)       Matangazo ya mikutano yatabandikwa katika ofisi ya Swissport SACCOS LTD na kwenye mbao za matangazo na vyombo vya habari, na kuwapa taarifa wanachama na kwa kutumia barua taratibu zinazokubalika sehemu hiyo.

 

b)       Muda wa matangazo ya mikutano:-

          a)       Mkutano Mkuu wa mwaka si chini ya siku 21.

          b)       Mkutano Mkuu wa kawaida si chini ya siku 14.

          c)       Mkutano Mkuu Maalum si chini ya siku 7.

 

12.4.  MAHUDHURIO KATIKA MIKUTANO

a)       Mahudhurio katika mikutano ya chama yatabidi kuwa si chini ya nusu ya wanachama wote au mia (100) ya wanachama hai ukichukulia idadi yoyote iliyo ndogo. Uwakilishi utakubalika kwa wanachama nje ya makao makuu, au utakapokubalika kutumika wakati wowote.

 

b)       Kwa mkutano mkuu ulioitishwa na Majis au Afisa aliyeteuliwa na Mrajis idadi yoyote ya wanachama waliohudhuria wataendesha mkutano na yoyote yatakayozungumzwa yatakuwa ni halali.

 

c)       Kwa mikutano mikuu ya mwaka na kawaida ikiwa mahudhurio hayatoshi baada ya saa moja na nusu ya saa zilizopangwa, mkutano utaahirishwa kwa siku saba (7), na mkutano uliohirishwa. Iwapo mahudhurio hayatatosha tena, mkutano wanachama waliohudhuria wanaweza kuendesha mkutano na maazimio yanaweza kutolewa na idadi isiyopungua nusu (1/2) ya wanachama na maamuzi yatakuw halali.

 

d)       Kwa mkutano uliotishwa na wanachama, mkutano utafutwa kabisa iwapo mahudhurio hayatatosha.

 

e)       Mwenyekiti wa Swissport SACCOS LTD ataendesha mikutano yote isipokuwa ule mkutano mkuu maalumu uliotishwa na Mrajisi ambapo Mrajis mwenyewe au mwanachama atakayemteua atakuw Mwenyekiti. Iwapo wote hawapo kwa muda wa dakika 30, mwanachama yeyote katika waliohudhuria atachaguliwa kuwa mwenyekiti wa muda ataongoza mkutano huo.

 

f)       Utaratibu ulivyo katika kanuni za vyama vya ushirika utapaswa kuzingatiwa katika kuendesha mikutano mikuu.

 

            12.3.1            USIMAMIZI

            12.3.2            HALMASHAURI YA SACCOS

a)       Halmashauri ya Swissport SACCOS LTD itachaguliwa na mkutano mkuu wa wanachama na wajumbe wote na kamati ya utendaji, kamati ya usimamizi na kamati ya mikopo watachaguliwa moja kwa moja toka kwa wanachama.

 

b)       Halmashauri ya Swissport SACCOS LTD itafanya mkutano angalau mmoja kila baada ya miezi mitatu.

 

c)       Halmashauri itapokea na kujadili taarifa za maendeleoya Swissport SACCOS LTD kutoka kwa kamati ya Usimamizi.

d)       Halmashauri ya Swissport SACCOS LTD itateuwa mwanachama atakayeshika nafasi iliyoachwa wazi katika kamati za Utendaji, Usimamizi na mikopo mkuu unaofuata ambapo nafasi zilizowazi zitajazwa kwa kura za wanachama.

 

e)       Katibu wa vikao vya Halmashauri atakuwa Meneja wa Swissport SACCOS LTD au katibu wa kuchaguliwa kama Swissport SACCOS LTD haijaajiri.

 

KAZI ZA HALMASHAURI NI PAMOJA:-

Kushirikiana pamoja kama timu katika kuendeleza chama cha ushirika kiuchumi na kijamii hususani:-

1.    Kuweka malengo ya jumla na sera za mwelekeo wa chama chao.

2.    Kuweka taratibu za mawasiliano na makubaliano mazuri kati ya wanachama na chama chao.

3.    Kuweka taratibu za uchunguzi wa halmashauri na kuweka bayana wajibu na madaraka ya halmashauri.

4.    Kueleza kinaganaga kazi, viwango vya mishahara na ajira za Meneja mkuu na kuandaa taratibu za kutathmini kazi na ufanisi wa Meneja Mkuu.

5.    Kuthibitisha muundo wa chama na ngazi za mishahara kwa ajili ya watumishi wa ngazi zote na kuidhinisha sera za utumishi na mipango  ya chama.

6.    Kuidhinisha mipango muhimu na mitaji ya kufanyia kazi.

7.    Kuidhinisha mabadiliko katika mali za chama.

8.    Kupendekeza mabadiliko katika masharti ya chama.

9.    Kushughulikia maombi ya kujiunga / kujitoa uanachama.

10. Kuandaa taratibu za kugawana ziada kulingana na jinsi kila mwanachama alivyoshiriki kw amujibu wa masharti ya chama.

11. Kuidhinisha kurudishiwa akiba / hisa kwa wanachama waliocha uanachama.

12. Kuweka taratibu za udhibiti (control) na kanuni za kulinda maslahi ya wanachama na wadai wengine.

13. Kuchambua na kutathmini maendeleo ya chama kulingana na malengo na madhumuni yaliyowekwa ili kuona iwapo yemefikiwa.

14. Kuhakikisha kuwa mikutano inaitishwa katika wakati unaotakiwa.

15. Kuandaa sera na mipango ya kudumu ya eleimu kwa ajili ya halmashauri ili iwe na muamko na ari inayotakiwa.

16. Kuandaa taratibu za mahusiano naushirika mzuri kati ya chama na vyama vingine vya ushirika ambayo vipo katika eneo hilo.

17. Kuunga mkono nakukisaidia chama chao kadri iwezekanavyo.

18. Katika chama cha akiba na mikopo halmashauri watahakikisha kuwa mikopo iliyotolewa inatumika kwa madhumuni iliyoombewa.

 

KAZI ZA MWENYEKITI

1.    Kujadiliana na kukubaliana na Meneja Mkuu kuhusu mambo yatakayowekwa katika agenda za mkutano.

2.    Atahakikisha kuwa taarifa za mikutano zimesambazwa ipasavyo kwa mujibu wa masharti ya chama.

3.    Atahakikisha kuwa wajumbw wote wa mkutano wanapewa kumbukumbu za majadiliano ya mikutano iliyopita.

4.    Atahakikisha kuwa Meneja Mkuu anaandaa taarifa ya maendeleo ya chama kibiashara

5.    Ataitisha na kuongoza mikutano yote ya wanachama na halmashauri kwa ufanisi kadri iwezekanavyo ili kutoa uamuzi wenye manufaa kwa chama.

6.    Atakuwa muweka sahihi katika mikataba yote kati ya chama na vyombo vingine vya nje.

 

KAZI ZA MENEJA / KATIBU

Kusimamia shughuli za SACCOS kulingana na miongozo iliyotolewa na halmashauri na kuwa Katibu wa Vikao vyote vya Halmashauri kama SACCOS imeajir na hususani:-

1.    Kuishauri na kuisaidia halmashauri kuweka maudhui, sera na malengo ya SACCOS.

2.    Kuangalia mwenendo wa mara kwa mara wa maendeleo ya chama na kuwaeleza halmashauri taaarifa na takwimu zitakazosaidia ili kufikia uamuzi wa busara ya kuandaa mipango.

3.    Kuandaa mipango muda mrefu na mfupi kwa kuthibitishwa na takwimu kwa ajili ya kuwasilisha kwenye mikutano ya halmashauri kufikia uamuzi wa busara.

4.    Kutekeleza sera na miongozo inayotolewa na halmashauri.

5.    Kuajiri na kuwasimamisha watumishi waliopo chini yake na kuwasiliana na halmashauri kwa ajili ya watumishi wa ngazi ya juu.

6.    Kuimarisha chama kwa kuwa na watumishi wa kutosha na kuandaa utaratibu wa maendeleo ya wtumishi.

7.    Atahakikisha kuwa fedha, huduma na mali zingine za chama zitatunzwa, zinawekewa bima na zinalindwa.

8.    Atahakikisha kuwa fedha, huduma na mali zingine za chama zinatunzwa, zinawekewa bima na zinalindwa.

9.    Kuimarisha uhusiano mzuri na mamlaka mbalimbali kuhusu wanachama na umma kwa ujumla.

10. Kushirikiana kikamilifu na vyama vingine vya ushirika.

11. Kuimarisha uhusiano mzuri na Mwenyekiti.

12. Kuonyesha uhusiano mzuri na Mwenyekiti.

13. Ataelekeza sera mpya ya utumishi na mpango wa maendeleo ya watumishi.

14. Atamuarifu Mwenyekiti kuhusu nani atakaimu shughuli zake wakati yeye meneja hayupo.

15. Atakuwa katibu / Muandishi katika mikutano yote ya wanachama nay a halmashauri.

16. Atakuwa muweka saini kwa mikataba mbalimbali kwa kushirikiana na mwenyekiti na halmashauri.

17. Atafanya kazi zingine za chama kadri atakavyopangiwa na halmashauri.

 

Kazi za halmashauri ni kutoa sera, malengo na miongozo mbalimbali kwa maendeleo ya chama. Kazi za menejimenti ni kutekeleza sera, malengo na miongozo ya halmashauri. Halmashauri haitakiwi kufanya kazi za menejimenti kwa kuwa kufanya hivyo ni kufuta taratibu za uwajibikaji wa menejimenti kw halmashauri na pia halmashauri kwa wanachama.

 

12.3.3      KAMATI YA UTENDAJI

a)       Kamati ya Utendaji itachaguliwa na mkutano mkuu miongoni mwa wajumbe wa mkutano mkuu Swissport SACCOS LTD.

 

b)       Wajumbe Kamati ya Utendaji watshika madaraka kwa muda wa miaka mitatu. Theluthi moja ya wajumbe watajiuzulu kila mwaka. Utaratibu wa kujiuzulu utapagwa katika mkutano wa kwanza mara baada ya kuandikishwa Swissport SACCOS LTD. Wajumbe wanaojiuzulu wanaruhusiwa kugombea tena nafasi zitakazokuwa wazi.

c)       Hakuna mjumbe atakayekuwa na haki ya kudai malipo ya mshahara au posho isipokuwa kama ilivyoelezwa katika masharti haya.

 

d)       Wajumbe wa kamati hii watakuw ani Mwenyekit, Makamu itakavyopagwa mara kwa mara. Katibu wa Kamati hii atakuwa Meneja wa Swissport SACCOS LTD kama Meneja ameajiriwa.

 

e)       Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ataacha madaraka kama akifukuzwa na Mkutano Mkuu / Kamati ya usimamizi au sababu yoyote kama ilivyo katika kanuni za vyama ya ushirika.

 

f)       Kamati ya utendaji inaweza kuchagua kamati ndogo ndogo kama itakavyoona infaa, kwa ajili ya utekelezaji bora zaidi wa kazi za Swissport SACCOS LTD.

 

g)       Mjumbe wa kamati hii atakayeshindwa kuhudhuria vikao vittu mfululizo bila ya sababu inayokubaliwa na kamati anaweza kuachishwa uongozi na kuteua mwanachama mwingine badala yake hadi mkutano mkuu unaofuata.

 

h)       Kamati ya utendaji itakuwa na mamlaka ya kusimamia shughuli zote za Swissport SACCOS LTD, mbali na majukumu mengine ya kamati hii itakuwa na wajibu wa kufanya mambo yafuatayo:-

 

i)        Kueneza elimu ya uwekaji akiba na utoaji mikopo, kuelimisha wanachama kuhusu matumizi bora ya mikopo yao.

ii)       Kupokea na kufikiria maombi ya wanachama wapya na kuyafikisha mbele ya mkutano mkuu unaofuata kwa uthibitisho.

 

iii)       Kuhakikisha kuwa wakopaji wanalipa madeni yao kama walivyoahidi na kuwachukulia hatua za kisheria wakopaji wasio waaminifu, na kupendekeza kwa mkutano mkuu ufutaji wa mikopo mibaya ambayo haiwezi kulipwa kabisa.

 

iv)      Kuweka utaratibu uendeshaji wa shughuli za akiba na mikopo ila kwa masharti kwamba taratibu hizo zisikiuke sheria na kanuni za vyama vya ushirka, masharti na maagizo ya Mrajis wa vyama vya ushirika.

 

v)       Kusimamia matumizi yote ya Swissport SACCOS LTD isipokuwa kazi za kuidhiisha maombi ya mikopo kulingana na masharti ya utoaji mikopo yaliyowekwa na Swissport SACCOS LTD na Mrajisi wa vyama vya ushirika.

 

vi)      Kuajiri, jusimamisha na kufukuza watumishi kazi kwa kuzingatia sheria za ajira zitakazotayarishwa na Swissport SACCOS LTD (Kanuni za Utumishi).

 

vii)      Kufikisha mbele ya mkutano mkuu wa mwaka mapendekezo ya makisio, hesabu ya mapato na matumizi, mizani na taarifa ya ukaguzi.

 

viii)     Kuandika na kutunza mihutasari ya majadiliano na maazimio yote ya mikutano ya kamati katika kitabu cha kumbukumbu za mikutano na kutiwa saini na Mwenyeki.

 

ix)      Kuendesha shughuli za Swissport SACCOS LTD katika misingi ya ushirika na kufidia hasar hiyo kama itakavyoamuliwa na Mrajis wa vyama vya ushirika, kwa mujibu wa sheria ya ushirika.

 

x)       Kusimamisha uanachama mwanachama au mjumbe yeyote wa halmashauri ya mikopo au ya usimamizi kutokana na tabia mbaya au kushindwa kutimiza wajibu wake wa kazi na kupeleka mapendekezo katika mkutano mkuu unaofuata ili uamuzi wa mwisho utolewe.

 

            12.3.4            KAMATI YA MIKOPO

a)       Maombi yote ya mikopo yatafikiriwa na Kamati hii. Itahakikisha kuwa mkopo unaoombwa ni wa manufaa kwa mkopaji. Itachunguza dhamana iliyotolewa kama ni sawa.

 

b)       Kamati hii itakuwa na wajumbe ambao watachuguliwa na mkutano mkuu.

 

c)       Wajumbe wa kamati watsshika madaraka yo kwa muda wa miaka mitatu. Theluthi moja (1/3) ya wajumbe itajiuzulu kila mwaka na wanaweza kuchaguliwa tena.

 

d)       Wajumbe wa kamati watachagua miongoni mwao, mwenyekiti na katibu. Kumbukumbu za mambo yote yatakayofanywa na kamati ni lazima nakala ziwe tayari kwa muda usiozidi siku tatu, tangu shughuli hizo zitendeke. Katibu wa kamati hii atakuwa Mhasibu kama Swissport SACCOS LTD imeajiri Mhasibu (idadi itategemea na mahitaji).

 

e)       Kamati hii itawajibika kufuatilia matumizi bora ya mikopo na kuhakikisha kwamba wakopaji wanatumia fedha kwa miradi au shughuli waliyoombea mikopo hiyo.

 

f)       Kamati itafanya kikao angalau kimoja  kila mwezi, lakini inaweza kufanya kikao cha dharura wakati wowote. Idadi ya juu ya jumla ya wanakamati wote itatosha kuendesha shughuli katika kikao. Hakuna wanakamati wote itatosha kuendesha shughuli katika kikao. Hakuna mkopo utakaotolewa pasipo kukubaliwa kwanza na wanakamati wote wa mkopo huo (isipokuwa kwa mikopo ambayo Afisa wa mikopo amepewa kibali). Taarifa ya vikao hivyo vitatolewa kwa wanachama katika mikutano yao mikuu.

g)       Kamati ya mikopo itachunguza kwa uangalifu tabia na hali ya fedha ya kila mwombaji kwa mkopo pamoja na dhamana, kama zipo na, kuhakikisha uwezo wa kulipa deni kwa ukamilifu katika muda uliowekwa. Kamati ya mikopo itawasaidia wakopaji katika kuondoa matatizo yao ya kifedha.

 

h)       Kwa wingi wa kura, kamati ya mikopo inaweza kumchagua Afisa au maofisa wa mikopo, kufanya kazi kama itakavyohitajika na kamati na kumpa uwezo wa kuidhinisha mikopo kwa kadri ya kiasi kinachowekwa na kamati. Hataweza kuchaguliwa zaidi ya afisa mmoja wa mikopo kutoka kwenye kamati. Kila afisa mikopo atatoa uliokataliwa naye kwa muda usiozidi siku saba tangu siku ya maombi yaliyopokelewa. Mikopo yote isiyoidhinishwa na afisa mikopo, itashughulikiwa na kamati ya mikopo. Hakuna mtu yeyote atakayekuwa na mamlaka ya kulipa kutoka mfuko wa chama hiki, mkopo usiodhinishwa na kamati ya mikopo au afisa mikopo (kwa SACCSOS ambayo ina muhasibu au Meneja atakuwa afisa wa mikopo).

 

            12.3.5            KAMATI YA USIMAMIZI

a)       Kamati ya usimamizi itakuw na wajumbe watakaochaguliwa na mkutano mkuu. Wajumbe wa Kamati hii lazima wawe wenye maadili mema, wapenda haki, wanaweza kusimamia kazi na kuchukua hatua za kurekebisha dosari pasipo upendeleo (Idadi itategemea na mahitaji).

 

b)       Wajumbe wa Kamati hii watshika madaraka kwa muda wa miaka mitatu na theluthi moja (1/3) ya wajumbe itajiuzulu kila mwaka na wanaweza kuchaguliwa tena.

 

c)       Wajumbe wa kamati hii watatengeneza utaratibu wa kutekeleza kazi za kamati hii ya usimamizi. Watachugua mwenyekiti na katibu miongoni mwao. Mwandishi atatengeneza na kuhifadhi kumbukumbu zote pamoja na hatua zinazochkukuliwa na kamati hii.

d)       Kamati itafanya kazi zifuatazo:-

i)        Kusimamia fedha na mali zote za SACCOS kwa niaba ya wanachama.

ii)       Kusimamia utekelezaji wa shughuli zote za Swissport SACCOS LTD na kuhakikisha kuwa zinafanywa ipasavyo.

 

iii)       Itatoa au itaamuru ufanyike japo mara moja katika miezi mitatu uchunguzi wa shughuli za DAHACO SACCOS LTD pamoja na ukaguzi wa vitabu itatengeneza au itaamuru utengenezaji wa taarifa itakayotolewa kwa Mkutano Mkuu. Katika maandishi na itakagua au itaamuru ukaguzi wa mwaka ufanyike na taarifa yake itolewe kwa maandishi katika Mkutano Mkuu wa mwaka unaofuata.

iv)      Kamati itafuatilia maendeleo ya miradi mikubwa ambayo imepatiwa mkopo na Swissport SACCOS LTD mpaka wahusika wanapomaliza marejesho.

 

v)       Kutayarisha taarifa ya maandishi juu ya hali ya fedha na huduma zitolewazo kwa wanachama kwa Kamati ya Utendaji na Mkutano Mkuu na nakala kwa Afisa Ushirika wa Wilaya, Mkoa na SCCULT, kila miezi mitatu ya mwaka wa fedha wa Swissport SACCOS LTD.

 

          12.3.6            MUHASIBU / MTUNZA HAZINA

Swissport SACCOS LTD itaajiri mhasibu mwenye sifa na ujuzi wa kutosha mara baada ya kuandikishwa. Aidha mwnachama mmojawapo mwenye ujuzi wa utunzaji vitabu atajitolea kufanya kazi ya mweka hazina pia anweza akalipwa malipo kidogo. Halmashauri inaweza kumrushusu na kuidhinisha malipo hayo baada ya kuyaafiki kwa pamoja. Kazi za mweka hazina / mhasibu zitakuwa hizi zifuatazo:-

a)    Kuandika na kutunza vitabu vya hesabu na kumbukumbu nyingine za fedha. Kutunza fedha na mali za Swissport SACCOS LTD. Kufuata kanuni zote za fedha na uandishi wa vitabu.

b)   Kupokea fedha yote iingiayo ndani ya Swissport SACCOS LTD na kufanya malinganisho ya fedha iliyopokelewa na iliyolipwa kila siku.

c)    Kuandaa miradi na mipango ya maendeleo ya muda mfupi na mrefu ya Swissport SACCOS LTD.

d)    Kufanya malipo yote baada ya kupata kibali maalum ch akamati ya utendaji, kamati ya mikopo au afisa mikopo.

e)    Kufanya marejesho ya mikopo na faida.

f)     Kufanya malinganisho ya hesabu ya benki kila mwezi.

g)    Kutayarisaha orodha ya wadaiwa kila mwezi na kuwasilisha kwa kamati ya utendaji na kamati ya mikopo ambao watatoa uamuzi kuhusu hatua za kuwachukulia wanachama waliochelewesha madeni yao zaidi ya miezi mitatu.

h)    Kusaidia wanachama katika kujaza fomu ya maombi ya mikopo na kuziwasilisha kwa kamati ya mikopo ili zifikiriwe. Financial na nakala kwa afisa ushirika wilayani, mkoani na Mrajis wa vyama vya ushirika.

i)     Kutia saini katika hundi za Swissport SACCOS LTD.

j)     Kusimamia shughuli zote za kila siku ndani ya Swissport SACCOS LTD zihusuzo fedha na kuwa katibu wa vikao vya kamati ya mikopo kama mhasibu aliyeajiriwa na afisa mikopo wa Swissport SACCOS LTD.

 

SEHEMU YA KUMI NA TATU k(13)

13.0   UDHINISHAJI WA UWEKAJI SAINI KUMBUKUMBU ZA SWISSPORT SACCOS LTD

Kumbukumbu zote na mikataba ya Swissport SACCOS LTD itasainiwa na mwenyekiti, au makamu mwenyekiti, kama mwenyekiti hayupo, katibu / Meneja na kama mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti hayupo basi mjumbe mmoja wa Halmashauri.

 

 

SEHEMU YA KUMI NA NNE (14)

14.0   UKOMO WA MADENI

Mkutano Mkuu wa Swissport SACCOS LTD lazima uweke mfumo wa madeni na ambao utaidhinishwa na Mrajis Msaidizi wa vyama vya ushirika kama ilivyo kwenye sheria ya ushirika.

 

SEHEMU YA KUMI NA TANO (15)

15.0   MUHURI WA SWISSPORT SACCOS LTD “COMMON SEAL”

15.1    a)       Swissport SACCOS itakuwa na “Common Seal” na muhuri huo utakuwa na

jina kamili la chama “Swissport I Savings and Credit Cooperative Society Ltd” na itakuwa tofauti na mihuri ya kawaida ya Swissport SACCOS LTD.

 

b)       “Common Seal” itatunzwa kwenye safe na kutumika na wahusika wakuu tu wnao saini kumbukumbu za Swissport SACCOS LTD.

 

SEHEMU YA KUMI NA SITA (16)

16.0   MAPENDEKEZO YA MASHARTI

Mashriti haya yatafanyiwa marekebisho kulingana na sheria ya ushirika na marekebisho hayo hayatakuwa halali hadi hapo yatakapoidhinishwa na kuandikishwa na Mrajisi wa vyama vya ushirika.

 

SEHEMU YA KUMI NA SABA (17)

17.0     KUVUNJWA, KUFUTWA NA KUFUNGWA KWA SWISSPORT SACCOS LTD

Swissport SACCOS LTD itaweza kuvunjwa na kufungwa kwa sababu zifuatazo:-

a)    Ka maombi ya wanachama wasiopungua ¾ ya wanachama wote.

b)   Iwapo wanachama wamepungua na kuwa chini ya kumi (10).

c)    Kwa amri ya Mrajis wa vyama vya ushirika chini ya sheria ya vyama vya ushika na marekebisho yake.

 

SEHEMU YA KUMI NA NANE (18)

18.0     MENGINEYO

a)    Mgogoro au malalamiko yoyote kuhusu masharti au huduma za Swissport SACCOS LTD kati ya wanachama au wanachama wa zamani au watu wanaodai kupitia SACCOS Halmashauri au Afisa yeyote au kati SACCOS na SACCOS au kati ya SACCOSS na chama kikuu (SCCULT) yapelekwe kwa mrajis wa vyama vya ushirika.

b)   Masharti haya yatasaidiwa na viambata au visaidizi kama vile kanuni za fedha (Financial Regulation) kanuni za UTUMISHI / Scheme of Service), sera na utaratibu za mikopo (Loan Policy and Procedure) na kanuni za uhasibu (Accounting manual).

2 comments:

  1. Very nice, keep it up. I love Corporative Societies.

    ReplyDelete
  2. Nataka kukuwa kwa namna ya uwanachama,ni Mtanzania tu ndiye anatakiwa kuwa mwanachama wa kundi lenu?
    Na ni kiasi gani cha pesa kinachoitajika kwa mtu kujiunga na Swiss Saccos ?
    Fomu zakujiungazinapatikana kwenye tovuti yenu au ni kuomba ofisini?
    Natamani kuwa mwanachama wenu nikibahtika kupata maelezo zaidi ya chama chenu mu lugha ya kiswahili.

    ReplyDelete